January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla apokea vifaa vya kampeni ya usafi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA kupatia ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali na kutoa onyo kwa Maduka yanayonunua dawa za Wizi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Mafunzo ya siku tano kwa Wakaguzi wa Dawa wa Manispaa za Mkoa huo yaliyolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa.

Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeji wa kazi hiyo ambayo inabeba *dhamana ya Maisha na uhai wa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka Wanaofanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawaÂ