Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo amefanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Mitaa ya Sharif, Madege na Mwasonga ambao Baada ya utafiti kufanyika maeneo yao yamebainika kuwa na Madini ambapo ameelekeza kila mtaa kuunda Kamati ya kujadili kiwango cha Fidia wanayohitaji kulipwa ili kukabidhi eneo kwa Mwekezaji na Mkoa utaunda Kamati ya kutafuta muafaka wa pamoja wa Jambo hilo.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo Baada ya kubaini mchakato Uliofanyika awali haukuwa Shirikishi Jambo lililosababisha Wananchi kutokubaliana moja kwa moja na kiwango Cha fidia kilichopendekezwa ambapo Mwekezaji alitoa Mapendekezo ya kulipa Tsh 3,000 kwa Mita moja ya mraba kiwango ambacho Wananchi wameona hakiendani na thamani ya Ardhi.
Kutokana na hilo RC Makalla amesema Kamati hizo zitakuwa na Wajumbe wakiwemo Wawakilishi wa Wananchi, Wataalamu wa Ardhi, Wanasheria na upande wa Mwekezaji na zitatakiwa kukamilisha kazi ndani ya wiki mbili na Baada ya hapo watampatia Mapendekezo ili aweze kutoa maamuzi ya Serikali.
Aidha RC Makalla amesema lengo la Serikali ni kuona Wananchi wananufaika kupitia Uwekezaji huo na Mwekezaji nae ananufaika na Serikali inapata Kodi.
Kwa upande wao Wananchi kwa pamoja Wamesema wapo tayari kupisha eneo kwaajili ya Uwekezaji lakini wanachoomba wapatiwe fidia inayoendana na thamani ya Ardhi na waweze kufidiwa Nyumba, Mazao na uendelezaji wowote Uliofanyika.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa