May 27, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

LHRC wazindua mradi wa majaribio

Na Mwandishi wetu, TmesMajira Online

KITUO Cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimezindua mradi wa majaribio ambao unalenga kuzuia na kukabiliana na udhalilishaji na unyanyasaji wa kingono

Mradi huo ambao utakuwa chini ya LHRC pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) utatekelezwa katika hospitali ya Rufaa Mwananyamala na Jamii inayoizunguka zikiwemo kata za mwananyamala na Makumbusho.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Mkurungezi Mtendaji LHRC, Anna Henga amesema mradi huo
utasaidia kujenga uwezo na kuhamasisha wadau mbalimbali ili kuweza kuzuia na kukabiliana na chagamoto za matukio ya udhalilishaji wa kingono kwa makundi mbalimbali.

Amesema hatua ya kuanzisha mradi huo imekuja baada ya LHRC kufanya utafiti mwaka 2019/2021 ambapo ilibaini kuwa vitendo vya uzalilishaji na ukatili wa kingono katika wilaya ya Kinondoni vimeongezeka.

” Kupitia utafiti huo tuliweza kubaini uwepo wa matukio 57,626 na Kati ya hayo mengi yalikuwa ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia hasa uzalilishaji wa kigono”amesema Henga

Alibainisha kuwa kwa mwaka 2020 ilikusanya matukio 448 ya mimba za utotono ambayo yalilipotiwa katika mikoa 15 ya Tanzania Bara katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Disemba huku matukio mengi yakiusisha wasichana wenye umri wa miaka 13 hadi 17.

Henga amesema jamii inapaswa kutambua kuwa vitendo vya unyanyasaji na uzalilishaji wa kingono ni kosa la Jinai kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya Jinai sura ya 16 kuanzia kifungu cha 130.
.

Akitaja baadhi ya wadau ambao watashiriki katika mradi huo ni pamoja madiwani, wenyeviti na watendaji wa Serikali za kata na mitaa, dawatu la polisi la jinsia na watoto, Maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii ngazi ya Mkoa, Manispaa na kata, pamoja na Asasi za kiraia pamoja na wadau ambao wengine.

Aidha amesema mradi huo utausisha upembuzi wa awali ili kubaini halihalisi ya uzalilishaji na unyanyasaji wa kingono, kujenga uwezo kwa watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, kufanya uhamasishaji kwa jamii inayoizunguka hospitali hiyo, kutoa msaada wa kisheria pamoja na kufanya tathimini fupi ya utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Mkono kwa Mkono, Asia Mkini alisema kituo hicho kilianza kufanya kazi mwaka 2009 ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 tayari kimetoa huduma kwa Watu 1000.

Amesema katika kituo kesi nyinyi ambazo wamekuwa wakipokea asilimia kubwa zimekuwa ni za watoto ambao wamefanyiwa ukatili ikiwemo uzalilishaji wa kingono.

” kesi tunazopokea katika kituo chetu zinahusiana na watoto kwa asilimia 84 huku zaidi ya nusu kesi tunazopokea zikiwa za udhalilishaji wa kingono”

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo hii