January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Kilimanjaro aonya tabia ya viongozi kutupiana lawama

Na Martha Fatael,TimesMajira Online,Same

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai ameonya tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali za mitaa kutupiana lawama na viongozi wa CCM wakati wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

Aidha Mkuu wa mkoa ametaka viongozi hao kushirikiana na kutoa taarifa pale wanapobaini baadhi ya miradi maendeleo inakwama kutokana na changamoto mbalimbali ili hatua zichukuliwe.

Amesema lengo la viongozi wa kada hizo ni ushirikiano wa pamoja katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 na kuona miradi inakamilika na wananchi wanapata maendeleo yaliyokusudiwa.

Akifungua semina kwa viongozi wa vijiji na kata kushirikiana na wale wa CCM Jimbo la Same Magharibi kwa ngazi hizo, Kagaigai alitaka kila upande kutekeleza wajibu wake.

Mapema akiwasilisha mada juu ya mahusiano ya Chama na serikali katika kutekeleza majukumu yao, Katibu wa CCM mkoani hapa,Jonathan Mabihya, alitaka viongozi kutumia staha kusahihishana.