Na Fresha Kinasa, Times Majira Online Mara.
MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amekabidhi magari matatu mapya yenye thamani ya Sh. Bil. 1,037,909,300 kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Gerald Kusaya.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Julai 31, 2026 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mbele ya watumishi mbalimbali.
Kanali Mtambi amesema, ununuzi wa magari hayo ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha utoaji wa huduma na kuchochea maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo.

Amesisitiza kuwa, magari hayo ni vitendea kazi muhimu vitakavyosaidia viongozi kufika kwa wananchi katika maeneo yote ya mkoa ili kutoa huduma.
“Naamini magari haya yatakuwa msaada mkubwa sana kuhakikisha mnawafikia wananchi katika maeneo yao na kuwapa huduma mbalimbali. Niwatake madereva na maafisa mtakaotumia magari haya kuyatunza na kuyatumia kwa matumizi stahiki yaliyokusudiwa,” amesema Kanali Mtambi.
Pia ameiishukuru Serikali kwa kuiwezesha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupata bajeti ya kununua magari hayo.
Magari hayo, yamenunuliwa kwa nyakati tofauti kupitia Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini – GPSA, kwa kutumia bajeti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Akizungumza mara baada ya kupokea magari hayo, Katibu Tawala Gerald Kusaya amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atahakikisha yanatunzwa na yanatumika ipasavyo katika kutoa huduma kwa wananchi.


More Stories
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki uzinduzi wa boti mpya za doria
Twange awataka wanasheria wa Tanesco kusimamia Maadili na Taaluma
Mchange ahoji Dkt.Nchimbi anajua madhara ya kauli zake