April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rashford, Sancho, Saka wakumbwa na ubaguzi wa rangi

LONDON, England

SHIRIKISHO la soka nchini Uingereza (FA), limelaani vikali ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya England, Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka baada ya timu hiyo kukubali kichapo dhidi Italia kwa mikwaju ya penalti 3-2, katika mchezo wa fainali kombe la Euro 2020 uliofanyika usiku wa kuamkia leo.

Wachezaji wote watatu walikosa kufunga mikwaju yao ya penalti jamo ambalo mashabiki waliwalenga katika mitandao ya kijamii, baada ya mchuano huo kumalizika.

Hata hivyo, Polisi wa eneo la Metropolitan wanachunguza ubaguzi huo na wamesema ‘Hautavumiliwa’ FA imesema ‘imeshangazwa’ na matusi hayo ya ubaguzi wa rangi. Wachezaji wa England wamekuwa wakipiga magoti katika michuano ya Euro kuangazia vita vyao dhidi ya ubaguzi wa rangi katik timu yao .

“Tutafanya kila tuwezalo kusaidia wachezaji walioathiriwa huku tukisisitiza adhabu kali zaidi kwa kila mtu anayehusika. “Tutaendelea kufanya kila tuwezalo kumaliza ubaguzi ndani ya michezo, lakini tunasihi serikali ichukue hatua za haraka na kuleta sheria inayofaa ili unyanyasaji huu uwe na adhabu za kudumu kimaisha kwa wahusika.

“Makampuni ya mitandao ya kijamii yanahitaji kuchukua hatua na kuwajibika kwa kuwapiga marufuku wanyanyasaji kutoka kwa majukwaa yao, kukusanya ushahidi ambao unaweza kusababisha kushtakiwa na kusaidia kufanya majukwaa yao kutotumiwa kwa dhuluma hizi’ Rashford aliangazia matukio ya kibaguzi aliyopokea kwenye mitandao ya kijamii mnamo Mei baada ya kupoteza fainali ya Ligi ya Uropa na Manchester United.

Na mwaka jana Sancho alikuwa miongoni mwa wachezaji nyota waliolalamika dhidi ya ubaguzi wa rangi kufuatia mauaji ya George Floyd na afisa wa polisi huko Minneapolis. Kampuni za mitandao ya kijamii zimekosolewa kwa kukosekana kwa hatua juu ya unyanyasaji wa kibaguzi kwenye majukwaa yao, na mnamo Aprili Instagram ilitangaza zana ya kuwezesha watumiaji kuchuja moja kwa moja jumbe za matusi kutoka kwa wale ambao hawawafuati.

Kufuatia matukio kadhaa ya unyanyasaji mitandaoni, vilabu kadhaa, wachezaji, wanariadha na mashirika ya michezo walishiriki katika siku nne za kususia mitandao ya kijamii mnamo Aprili kuhamasisha kampuni kuchukua misimamo mikali dhidi ya unyanyasaji wa kibaguzi na kijinsia.