May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RAS aagiza hatua za kinidhamu kwa watumishi

Na Tiganya Vicent, TimesMajira,Online Tabora

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wameagiza kuchukulia hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wote ambao wanaosihi nje ya vituo vyao vya kazi na kuendelea kuisababishia Serikali hasara na kuzorotesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Amesema tayari kuna orodha ya watumishi ambao bado wanaishi Tabora mjini badala ya kukaa katika eneo la Isikizya ambayo ni ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Uyui

Makungu amesema kuwa hivi sasa hakuna kisingizio kwa sababu upatikanaji wa huduma zote muhimu kama vile maji ya uhakika, umeme na afya zipo katika Makao Makuu ya Halmashauri hiyo.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Msalika Makungu akitoa maagizo jana wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Amesema kuendelea kwa Watumishi kuishi Tabora mjini huku wakifanyakazi Uyui ni dharau dhidi ya maagizo ya viongozi wa juu waliyoyatoa katika nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali hapa nchini ya kuzitaka Halmashauri zote ambazo Ofisi zake ziko katika Halmashauri nyingine kuondoka na kwenda kwenye makao makuu yao na watumishi wake.

Makungu amesema kama madiwani wakishindwa kuwachukulia hatua Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatarajia kuchukua hatua kali.

Ameongeza sanjari na Watendaji wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Uyui na watumishi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya wanatakiwa kuishi maeneo yao ya kazi.

Makungu amesema lengo la kuwataka watumishi wote katika maeneo yao ni kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu wakitaka huduma kutoka kwa watumishi kwa kisingizio ya kuishi mbali na Ofisi zao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Said Ntahondi alimtaka Mkurugenzi Mtendaji kuorodhesha majina ya watumishi wote ambao hadi hivi wanaishi nje ya Isikizya ili Baraza la Madiwani liweze kuwachukulia hatua za kinidhamu