Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online Mkurugenzi wa Ranchi ya Mbogo Pirmohamed Mulla (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb) nyaraka ya umiliki wa ng’ombe dume aina ya boran kwa serikali, baada ya ranchi hiyo kutoa msaada kwa serikali ili ng’ombe huyo atumike kuzalisha mbegu na kupandikizwa kwa ng’ombe jike ili kuboresha mifugo nchini. Makabidhiano hayo yamefanyia katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb) akimfanyia tathmini ng’ombe dume aina ya boran mwenye umri wa miaka mitatu ambaye ana kilogramu 624 na ana thamani ya Shilingi Milioni Sita baada ya serikali kukabidhiwa ng’ombe huyo kutoka Ranchi ya Mbogo, ambapo Waziri Ndaki amesema dhamira ya serikali ni kuhimilisha ng’ombe jike Laki tatu kwa mwaka wa fedha 2022/23, hivyo ng’ombe huyo atapelekwa katika Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzalisha mbegu. Waziri Ndaki amebainisha hayo baada ya makabidhiano ya ng’ombe huyo yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya. Post Views: 593 Continue Reading Previous Makumbusho ya Taifa yaja na zao jipya la utaliiNext DCEA yawataka wananchi kutembelea kwenye banda lao kupata Elimu ya utambuzi wa dawa za kulevya More Stories Habari Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi December 23, 2024 Judith Ferdnand Habari Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga December 23, 2024 Judith Ferdnand Habari Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini December 23, 2024 Hamisi Miraji
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini