May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Raisi Samia kufungua mkutano wa Majaji Oktoba 23 Arusha

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu hassani anatarajiwa kufungua mkutano wa mwaka wa majaji wakuu kutoka nchi za kusini na mashariki mwa Afrika jijini Arusha October 23

Aidha kabla ya mkutano huo wa majaji wakuu pia kutakuwa na kikao cha watendaji wakuu wa mahakama kitakachofanyika october 22

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo mtendaji mkuu wa mahakama hapa nchini, Profesa Elisante ole Gabriel Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ndio mwenyeji wa mkutano huo.

Profesa Ole Gabriel alidai kuwa Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa kuwa imeweza kupiga hatua kubwa kwenye sekta ya mahakama

“sisi ni mwenyeji wa mkutano huo na tunajivunia sana kwa kuwa nchi kupitia sheria ambazo zimewekwa zimeweza kutufikisha mbali na ndio maana sasa hata nchi nyingine nazo sasa zitakuja kujifunza kwetu”aliongeza

Profesa Ole Gabriel alisema kuwa katika mkutano huo watakuwa na mada kuu 3 ambazo zinazohusu jukwaaa hilo huku lengo likiwa ni kuendelea kuboresha na kuleta maslahi kwa nchi

Alitaja mada hizo kuwa ni pamoja na urekibishaji na uboreshaji wa katiba ya jukwaaa hili, mada ya pili ikiwa ni vyanzo vya chama hicho, huku mada ya tatu ni uwajibikaji na ushirikwaji kwa watendaji wakuu wa mahakama

Mbali na ufunguzi wa mkutano huo pia alisema kutakuwa muda mfupi kutoka sasa Tanzania inatarajia kuanza kupokea watalii kwenywe sekta ya mahakama ambapo tayari uwekezaji mkubwa sana ulishafanyika

“tuna jengo letu ambalo ni moja ya majengo sita makubwa ambapo hapo sasa wageni kutoka ngazi ya mahakama watakuja kujifunza Kutoka kwetu na sisi tunajivunia sana hilo kwa kuwa hata hao wageni wanapokuja uchumi unaimarika zaidi”aliongeza