January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia mgeni rasmi maonesho ya pili ya elimu na ufundi standi

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasani Leo anatarajiwa kufungua maonesho ya pili ya elimu na ufundi standi(NACTVET) Jijini Arusha huku lengo halisi la maonesho hayo ni kuonesha umma namna vyuo hivyo vinavyotoa elimu na ujuzi mbalimbali

Akiongea mapema Leo mratibu wa maonesho hayo Kutoka Nact Vet,Bw Twaha Twaha alisema kuwa maonesho hayo yameeanza Jijini Arusha Toka May 16 na yatafunguliwa rasmi na Raisi Samia

Twaha alisema kuwa maonesho hayo ambayo yameshirikisha wadau wa chuo,taasisi mbalimbali pamoja na wajasirimali ni moja ya maonesho ambayo yanaweza kuwapeleka watoto au vijana kufika kwenye ndoto zao ambazo wanazitaka

Alisema kuwa ndani ya maonesho hayo vyuo kama 170 vipo na lengo halisi la uwepo wa vyuo hivyo ni kutaka kutoa fursa Kwa jamii kuchagua aina ya vyuo ambavyo wanavitaka kwa mujibu wa ndoto zao

“Vyuo vinapokuwa hapa ni raisi sana kupata maelezo yake sanjari na vigezo lakini ni raisi hata Kwa kijana kuweza kuuliza kile ambacho anakitaka na kupata majibu sahihi Mimi nadhani kuwa Hii ni fursa kubwa Kwa wakazi wa Arusha pamoja na mikoa ya Jirani kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi”alisema

Katika hatua nyingine wakiongea Kwa niaba ya wafadhili wa maonesho hayo,

mdhamini mmojawapo ambaye ni chuo cha uhasibu Arusha,walisema kuwa maonesho hayo yamelenga kuboresha ndoto za vijana ambao mara nyingine huwa wanakosa ndoto zao Kwa kukosa taarifa sahihi hasa za vyuo

Castro Malimali ni mmoja wa wanafunzi WA chuo cha uhasibu Arusha ambaye pia ni msimamizi wa kiatamizi cha kibiashara ambapo yeye anasema kuwa maonesho hayo ya NACT VET yanatakiwa kuwa ya Kisumu ili hata hata baadhi ya vyuo pia viweze kuonesha KAZI zake ambazo zinafanywa na vijana

“Hapa kwenye Banda letu la chuo cha uhasibu Arusha tunaonesha namna vijana tulivyonufaika na programu Hii,sasa Hii inaweza kuibua mawazo mapya ambayo vijana wanao Kila siku,na wakija hapa watajifunza je kama maonesho yasingekuwepo ni fursa kubwa sana Kwa vijana”akiongea

Akiongelea mpango huo wa kiatamizi cha kibiashara alisema kuwa mpaja sasa vijana wengi sana wameshaweza kunufaika na mpango huo ambao wameweza kujiajiri sanjari na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama sera ya viwanda inavyo sema

Pamoja na hayo aliiomba Serikali kuangalia upya mchakato mzima wa usajili Kwa makampuni au biashara kwa wajasiriamli wachanga ambapo alidai kuwa kwa Sasa mlolongo ni mkubwa sana na wakati unafanya baadhi ya ndoto za vijana kuishia njiani.