May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kolandoto chawafundisha vijana utengenezaji madawa

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Vijana zaidi ya 350 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wamefanikiwa kupewa elimu na mbinu ya kutengeneza madawa Aina 80 kutoka katika chuo cha afya za sayansi Kolandoto

Vijana hao ambao wamepatiwa elimu hiyo ambayo pia ipo chini ya kozi ya ufamasia kutoka katika chuo hicho wamefanikisha maarifa hayo ya kiteknolojia ili waweze kwenda kutengeneza madawa Kwa kufuata sheria za nchi lakini pia naitaji ndani ya jamii.

Hayo yameelezwa na Bw Pascal Marusu ambaye ni Mkuu wa idara ya famasi Kwa niaba ya Mkuu wa chuo hicho wakati akiongea na waandishi wa habari mapema Jana kwenye maonesho ya NACT VET yanayoendelea Jijini Arusha.

Alisema kuwa program hiyo ilianza miaka minne iliyopita na imeweza kuwasaidia vijana wengi kuweza kujiajiri na hivyo kuongeza nguvu kubwa ya pato la Taifa

“Ndani ya programu Hii vijana ambao wameweza kupata Mafunzo hayo Kwa kweli tunajivunia sana kwa kuwa wameweza kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii”aliongeza

Katika hatua nyingine aliitoa wito Kwa wataalamu sekta ya afya kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuwa na maadili mema ambayo msingi wake huweza kuwa wataalamu Bora Kwa jamii

“Ndani ya chuo chetu Sisi tunawapa mikakati na mbinu ya kuwa na maadili ambayo ni chanzo cha utoaji wa huduma Bora kwenye jamii na tunajua hawa vijana hasa Wa sekta Hii ya afya wakiwa na maadili mema wataweza kuwa Bora makazini”aliongeza

Aliwataka Vijana hasa wenye ndoto za kujiajiri katika sekta ya afya kuhakikisha kuwa wanajiunga na chuo hicho na kupata Mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia kujiajiri ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Pascal Marusu ambaye ni Mkuu wa idara kutoka chuo cha afya ya sayansi akiwa mwanafunzi wa chuo hicho wakionesha baadhi ya dawa ambazo zimetengenezwa Kwa ajili ya matumizi ya binadamu,mapema Jana kwenye viwanja vya stadium katika maonesho ya NACT VET.