December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia azindua mradi wa maji Kyaka bunazi

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Missenyi

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,amezindua mradi wa maji wa Kyaka bunazi wenye thamani ya shilingi Bilioni 15.7 ambao utahudumia wananchi zaidi ya ( 65,470) wa Kata ya Kyaka na Kasambya.

Akiongea na Wananchi wa Missenyi,Rais Samia Hassan,alisema mradi huo ni kielelezo Cha serikali jinsi inavyoendelea kutekeleza miradi mbalimbali lengo likiwa kufikisha huduma muhimu kwa jamii.

Alisema watahakikisha wananchi wanapata maji Safi na salama wakati wote.

Hata hivyo ametoa maelekezo kwa waziri wa maji Juma Aweso na katibu mkuu wa wizara hiyo Antony Sanga kukopesha mamlaka za maji za Kyaka bunazi kiasi Cha shilingi Milioni ( 500 )ili iwe nyenzo ya kuwaunganishia maji haraka wananchi.

Alisema baada ya kuunganishiwa maji wananchi hao watapaswa kulipa hizo fedha ili zipelekwe mamlaka nyingine pia wananchi waweze kupata huduma za kuunganishiwa maji .

Aliwataka wananchi pia kutunza vyanzo vya maji ukiwemo mto Kagera.

Awali katibu mkuu wa wizara hiyo Sanga,alisema mradi huo una uwezo wa kuzalisha lita za maji Milioni 8.2 wakati mahitaji ni Milioni 5.2.

Alisema jumla ya wateja 900 wameshaunganishiwa maji kutoka katika mradi huo.

Alisema huo ni mradi mkubwa kutokea katika mto Kagera haujawahi kutokea kabla.

Naye waziri wa maji ,Juma Aweso,alisema wananchi wa Missenyi walipoteza ndugu zao kutokana na kukosekana kwa maji baada ya kuliwa na mamba mto Kagera.

Waziri Aweso, alisema wananchi hao walikuwa wanapata maji kidogo asilimia 20 tu.

Alisema ni haki ya mwananchi kupata huduma ya maji na yeye wajibu wake ni kulipa bili halali ya matumizi yake sio kubambikiwa bili.

RAIS Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji Kyaka Bunazi