Na Penina Malundo, TimesMajira Online
Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya kumpatia mtaji wa Biashara na fedha za kujikimu Yassin Said mwenye Ulemavu wa Ngozi ambaye aliemuandikia barua Rais Samia akiomba kuwezeshwa kiuchumi baada ya kupitia masaibu katika maisha yake.
Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya *Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemsisitiza Kijana huyo kutumia fedha alizopatiwa kujiimarisha kiuchumi ili lengo la Rais Samia kutoa fedha hizo liweze kutimia.
Kwa upande wake Said amemshukuru Rais Samia kwa msaada aliopatiwa na kuahidi kuzitumia fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa.

More Stories
Mzumbe yatekeleza miradi ya bil.15.66/- kuimarisha elimu
Dar yajipanga kupokea washiriki 12000 Jukwaa la Africa50
Mwanafunzi abuni Lishe Bora kupambana na utapiamlo