Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea leo asubuhi baada ya gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kugongaba na Daladala.
Salamu hizo zinasema;
“Nimeshtushwa na vifo vya Watu 14 wakiwemo Wanahabari 6 vilivyotokea leo asubuhi baada ya gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kugonga na Daladala. Poleni Wafiwa, Wanahabari na jamaa wote. Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu na Majeruhi wapone haraka.”
Kuhusu taarifa hiyo ya ajali inasema
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Emmanuel Luponya Sherembi, ameahirisha ghafla ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali iliyotokea saa chache na kusababisha vifo.
“Mkurugenzi Mtendaji anasikitika kuwafahamisha kuwa, ratiba ya ziara ya leo ya kukabidhi miradi yetu kwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeahirishwa ghafla.
“Hii ni kutokana na ajali mbaya iliyoukumba msafara wa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wakati akiwa anakuja ambapo gari lilokuwa limebeba kikosi cha waandishi wa habari limegongana na Hiace uso kwa uso maeneo ya Busega.
“Taarifa zinasema kuwa watu watano wamepoteza maisha ambao inasemekana kuwa ni waandishi na maafisa habari ndani ya mkoa wetu na pia inasemekana kuwa mojawapo ya waliofariki ni pamoja na ofisa habari na mahusiano wetu, Bw.Stephen Msengi.
“Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na kuthibitishwa. Kufuatia hali hiyo, uongozi wa mkoa na wilaya umeamua kusitisha ratiba ya ziara hii hadi siki nyingine itakayopangwa.Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen”
Taarifa za awali zilizotolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko imeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Busega, Simiyu na kwamba waandishi wa habari watano wamepoteza maisha katika ajali hiyo.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua