January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia aamsha shangwe za Machinga baada ya kuongea nao wakiwa mafunzoni

Na Joyce Kasiki,Timesmajiraonline,Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan amemsha shangwe za viongozai wa Shirikisho la umoja wa Machinga (SHIUMA)  baada ya kupiga simu ya kiganjani na kuongea na machinga waliokuwa wakiendelera na mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo viongozi wa machinga yanayoendelea jijini Dodoma.

Akizungumza na viongozi hao wa SHIUMA,Rais Samia ameahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa kila mkoa ili ziweze kusaidia shughuli za uendeshaji wa ofisi.

Hatua hiyo iliwafanya Machinga kupiga kelele za shangwe na kuimba nyimbo mbalimbali za kumsifia Rais kwa kuonyesha moyo huo wa kuwajali.

Rais Samia alitoa ahadi hiyo kupitia simu ya mkonni ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima mara baada ya Naibu Katibu Mkuu wa SHIUMA  Josephu Mwanakijiji kusoma risala yao iliyoeleza changamoto katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa yakirushwa mubashara.

“Watoto wangu,kundi langu nimefuatilia mkutano wenu,nimesikia vchangamoto zenu,nashukuru Waziri kwa kuwapa ofisi katika Jengo la Serikali ,sasa kuanzia Julai Ofisi ya Rais  itatoa milioni 10 kwa kila Mkoa,”alisema Rais Samia

Mwanakijiji alitumia pia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kuliona kundi la Machinga ni muhimu kwani mpaka sasa Wizara hii imekuwa kiunganishi kikubwa baija yao na Serikali.

“Pamoja na changamoto zinazotukabili,lakini Wizara hii imejitahidi kuweka mifumo mizuri ya kiutendaji ili baadae tuwe wafanyabiashara wakubwa imani yetu changamoto za Machinga zitapungua.”alisema

Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima  amewapa  Machinga mbinu mpya za kisasa ili waweze kupata matokeo chanya ambayo yataleta maendeleo ya Machinga na Taifa kwa jumla.

Aidha Waziri Gwajima amewataka viongozi hao kuwaheshimu viongozi wa ngazi ya wilaya na mikoa lakini pia wafuate taratibu ili changamoto zao ziweze kutatuliwa.

“Naomba mfuate kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa amani bila kubugudhiwa na vyombo vya usalama katika maeneo yenu.”alisema Dkt.Gwajima

Naye  Naibu Waziriwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum  Mwanaidi Ali Hamis amesisitiza Wamachinga wote bchini  kwenda sambamba na jitihada za Serikali ili kuleta maendeleo chanya. Awali