Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza (55), amefariki kwa mshtuko wa moyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, Nkurunziza ambaye amemaliza muda wake wa urais mwaka huu, amefariki katika hospitali ya Karusi alipokuwa amelazwa jana.
Kulingana na msemaji wa Serikali, Balozi Willy Nyamitwe, Rais Pierre Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo kinyume na uvumi unaoenezwa. Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezi na alituma salamu za ramirambi kwa familia.
Rais Pierre Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1963 Mwansiasa wa Burundi na amekuwa madarakani tangu 2005, akiwa amedumu madarakani kwa miaka 15.
Awali alikuwa Mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama Rais wa Burundi. Mwaka 2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu ofisini.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito