December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Magufuli: Mwenyekiti wa CWT aliomba mishahara ilipwe wakati shule zimefungwa

Na Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli amesema hampigii debe Mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Walimu Leah Ulaya, ila yeye ndio aljyepiga simu na kuniomba niwalipe walimu kipindi hiki chote cha Corona.

Amesema alipiga simu asubuhi muda mrefu ambapo ilipokelewa na wasaidizi wake wakidai anahitaji kuongea naye.

“Mimi na nilipopewa simu ndo nilisikia akiomba nisifanye kama nchi nyingine niwasaidie walimu kuwalipa mishahara yao kipindi hiki cha Corona” amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema alitafakari ombi hilo na baadae kuamua kuwa walimu wataendelea kulipwa kipindi chote cha ugonjwa wa  Corona hata kama corona ikiwepo mwaka mzima au miaka 10.

Amesema sekta ya elimu ni sekta mama na corona haijaletwa na walimu.