Na Mwandishi Wetu
Rais John Magufuli amesema hampigii debe Mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Walimu Leah Ulaya, ila yeye ndio aljyepiga simu na kuniomba niwalipe walimu kipindi hiki chote cha Corona.
Amesema alipiga simu asubuhi muda mrefu ambapo ilipokelewa na wasaidizi wake wakidai anahitaji kuongea naye.
“Mimi na nilipopewa simu ndo nilisikia akiomba nisifanye kama nchi nyingine niwasaidie walimu kuwalipa mishahara yao kipindi hiki cha Corona” amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema alitafakari ombi hilo na baadae kuamua kuwa walimu wataendelea kulipwa kipindi chote cha ugonjwa wa Corona hata kama corona ikiwepo mwaka mzima au miaka 10.
Amesema sekta ya elimu ni sekta mama na corona haijaletwa na walimu.

More Stories
Mbeya City Expo yaelimisha wananchi bidhaa bandia
TASAC ,NBS zashirikiana sensa vyombo Majini
Kihongosi:Viongozi msitunishiane misuli