Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuadhimisha miaka 56 ya Muungano, Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,973.
Kati ya wafungwa hao, 3,717 wamesamehewa vifungo vyao, na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.
Kupitia salamu zake za maadhimisho ya Muungano, Rais Magufuli amesema ana matumaini kuwa wafungwa hao wamejifunza na watajirekebisha ili waungane na jamii katika kulitumikia Taifa wakiwa raia wema wanaozingatia sheria na taratibu.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi