Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu David Cleopa Msuya kilichotokea leo tarehe 07 Mei, 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Taarifa zaidi ya Mipango kamili ya msiba itaendelea kutolewa na Serikali.
Rais Dkt. Samia ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 7 hadi 13 Mei, 2025.
Rais Dkt. Samia anawapa pole Ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba huu.

More Stories
Zungu achaguliwa kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa IPU
Dkt.Homera azindua mkataba mpya wa huduma TANESCO
Dkt.Homera aitaka TANESCO kuboresha kasi ya huduma