Na Mwandishi Wetu,Pwani
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Kibaha Mjini wilayani ya Kibaha mkoani Pwani wamedai kuwa uchaguzi wa ndani wa chama hicho ulitawaliwa na vitendo vya rushwa na kusababisha wajumbe kupitisha viongozi wasiokuwa waadilifu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi na wananchi wa eneo hilo walidai kuwa kuna haja ya kubadilisha utaratibu wakuchagua viongozi hao kutoka kutumia wajumbe badala yake watumie wanachama wa kawaida kwakuwa kundi linalochagu viongozi ni watu wachache na rahisi kupewa rushwa.
Mmoja wa wanachama hao ambaye ni diwani mstaafu wa kata ya Msangani Genze Chongela alisema katika uchaguzi huo hatua za awali zilienda kwa haki, lakini wakati wa kupiga kura hakukuwa na haki kwa sababu rushwa zilitembea sana kwa wajumbe.
“Hawa wajumbe wa nyumba kumi tunaowatumia ni rahisi sana kupewa rushwa ilifika mahali watu wanapewa hadi laki laki za rushwa kwa muda mmoja.
“Hakuwezi kuwa na uchaguzi bado mgombea mmoja (jina tunalo) alishasema ametenga Sh Milioni 200 kwa ajili yakuangusha madiwani ambao hawapo upande wake,kila ambaye alikuwa hatetei maslahi yake alikatwa,”amesema Chongela.
Amesema huku akitolea mfano kwake ambapo anadai uadui na mtia nÃa huyo ulianza baada ya yeye yakumuoa adui yake.
“Alishasema ataweka Sh Milioni 200 kuning’oa kisa nilioa mtu ambaye nk adui yake na nimeangushwa na kweli,aliapa madiwani wote waliopinga shughuli zake zakimaslahi wataondoka na alihakikisha wote kumi hatujachaguliwa,”amesema Chongela.
Naye Mjumbe wa shina naba nane, Ramdhani Ngoda alisema hajaridhishwa na mchakato huo kwakuwa rushwa ilitumika kwa kiasi kikubwa kufadhili watu waangushwe.”Sisi kilio chetu tunakipeleka kamati kuu kutokanana uchafu huu wanapaswa kuangalia mtu sahihi kuanzia kwenye ubunge hadi madiwani ili waweze kumrudisha kwa wananchi ili apeperushe bendera ya chama,”amesema Ngoda.
Amesema hajaridhishwa na uchaguzi huo.”Nimepiga kura lakini katika kupiga kura sikufurahishwa .Sisi tuna mikutano tisa,mikutano mitatu tunafanya kila baada ya miezi mitatu,mkutano unamtaka madiwani na wabunge wawepo pamoja na wanachama wanatakiwa waje watoe maoni, lakini wengine hatuwaoni lakini wanakuja kipindi cha uchaguzi tu wanashinda ,”amesema Ngoda.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako