Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Sabasaba
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanzisha mfumo wa kisasa wa kutoa huduma kwa wanachama wake kupitia njia ya mtandao popote wanapkuwa yaani (online portal).
Mfumo huo umeanzishwa na mfuko huo ikiwa ni miaka miwili tangu kuanzishwa kwa mfuko.
Mhandisi wa Mifumo ya Kompyuta (System engineer) wa Mfuko huo, Goodluck Msangi, ameeleza jinsi mfumo huo unavyofanya kazi kwenye Banda la PSSSF lililopo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa maarufu kama Sabasaba.
Mhandisi Msangi amesema mfumo huo unawawezesha wanachama na wastaafu kupata taarifa mbalimbali kuhusu mwenendo wa michango na taarifa za malipo ya pensheni ya kila mwezi.
“Kwa wanachama wanaweza kupata taarifa ya mwenendo wa michango yao iliyowasilishwa na mwajiri, mstaafu ataweza kupata taariza za malipo ya pensheni ya mwezi kiasi kilicholipwa benki.
Pia mfumo huo unawezesha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mwanachama au mstaafu na mfuko wakati wowote na mahala popote bila ya muhusika kuhitajika kufika kwenye ofisi za Mfuko.” Amefafanua mhandisi Msangi.
Aidha kupitia mfumo huo endapo mwanachama ana maoni, ushauri au anahitaji ufafanuzi wa jambo lolote anaweza kufanya hivyo na mrejesho atapata mara moja.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati