April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Popat: Bado tuna jambo letu, tunaitaka Ligi Mabingwa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

OFISA Mtendaji Mkuu wa klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema watapambana hadi mwisho ili kuhakikisha wanachukua alama tatu katika kila mchezo ulio mbele yao na kukaa katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ili kupata uwakilishi katika michuano ya Ligi Mabingwa Afrika msimu ujao.

Hadi sasa katika michuano hiyo Tanzania ina zaidi ya asilimia 90 kuingiza timu nne katika mashindano ya kimataifa ambapo timu tatu za juu katika msimamo wa Ligi zitashiriki Ligi Mabingwa Afrika huku mshindi wa kombe la Shirikisho la Azam ‘Azam Sports Federation Cup’ akiiwalikisha nchi kwenye michuano ya Shirikisho Afrika.

Baada ya juzi timu yake kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Yanga lililofungwa dakika ya 86 na Prince Dube na kukaa kileleni mwa orodha ya wafungaji bora msimu huu akiwa na goli 12, Popat amesema kuwa, Azam bado wana jambo lao msimu huu na watahakikisha wanapambana katika mechi zilizosaili ili kulifikia.

Amesema, ushindi dhidi ya Yanga umewafanya kufikisha alama 54 lakini pia umewaongezea morali ya kupambana zaidi kwani ukiangalia aliyekaa kileleni amewazidi alama nne hivyo bado wapo kwenye mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

Amesema kuwa, hadi sasa ukiangalia katika msimamo wa Ligi ni ngumu kutabiri nani atakuwa bingwa na ukiangalia timu zote tatu za juu zinabimbizana kutwaa ubingwa huo hivyo kikubwa ni kujipanga ili kufanikisha jambo lao.

Wao kama timu siku zote wamekuwa wakijipanga na kugombea nafasi ya ubingwa kila msimu ingawa mara nyingi mambo huenda mrama mwishoni.

“Mpira una changamoto nyingi na hapa katikati tumepitia wakati mgumu baada ya kutetereka kalini sasa tumekaa san ana mkakati wetu ni kuhakikisha tunaendeleza morali hii katika mech izote zilizosalia ambazo tunahitaji kuchukua alama tatu katika kila mmoja,”

“Kikubwa ni kujipanga kwani ikiwa hatutatwaa ubingwa basi kukaa katika nafasi ambayo tyunaweza kuapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa na ikiwa hilo litafanikiwa basi mkakati wetu ni kwenda kufanya vizuri kama ilivyo kwa Simba,” amesema Popat.

Katika hatua nyingine kinara wa mabao ndani ya Azam na Ligi Kuu Dube amesema kuwa, kikubwa kilicho mbele yake kwa sasa ni kuangalia ni namna gania ataweza zaidi kuifungia timu yake ili kuipa mafanikio wanayoyahitaji.

Amesema, kila mchezaji anatamani kuwa mfungaji bora wa msimu lakini kwake hafikirii sana jambo hilo na ndio maana goli alilofunga katika mchezo dhidi ya Yanga ni zawadi kwa wachezaji wenzake ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kushirikiana.

“Kila mshambuliaji dhamira yake ni kushinda kiatu cha dhahabu lakini kwangu kwa sasa jambo kubwa ni kuanagalia ni namna gani ninaweza kuipambania timu yang una nashukuru sapoti ya wachezaji wenzangu ambayo leo imeniweka hapa,” amesema Dube.