Na mwandishi wetu,TimesMajira online Bukoba,
WAPIGA kura wowote watakaokwenda kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu Octoba 29 ,mwaka uu hawatang’atwa na sisimizi wala kunguni kwenye barabara zote watakazopita watakuwa salama wakati wa zoezi hilo.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kagera Blasius Chatanda, wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake leo.
Kamanda Chatanda, amesema ikiwezekana barabara hizo atazifagia na kuzipiga deki ili wananchi wanaokwenda kupiga kura wapite kwa amani na utulivu.
Amesema wananchi wasiwe na hofu katika zoezi la kupiga kura anawahakikishia usalama wao hakuna atakayewagusa.”Sote tunatambua kwamba zoezi hili ni la kikatiba na ni demokrasia ya kila mmoja wetu na haki ya kila Mtanzania kushiriki katika uchaguzi mkuu, tunawahakikishia watakaoenda kupiga kura kuwa amani na utulivu wa kutosha umeimarishwa maeneo yote ya mkoa wa Kagera “anasema kamanda Chatanda.
Ameongeza kuwa jeshi hilo limejipanga kuanzia nchi kavu hadi majini hasa maeneo ya visiwani kuna bodi zaidi ya 11 na magari ya kutosha kila Kata sanjari doria za kutosha ziwani na nchi kavu na Askari wa kusimamia vituo vya uchaguzi wapo tayari wanasubiri muda ufike.
Pia amesema jeshi la polisi limejipanga liko imara na limesimama madhubuti kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu .Hata hivyo alitoa onyo kwa baadhi ya wananchi hasa vijana wanaofikiria kuanzisha vurugu siku ya kupiga kura wasithubutu kwa sababu hawatapata hiyo nafasi jeshi la polisi limejipanga kikamilifu.
Amesema watakaojaribu kuingia barabarani watashughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
Anatoa wito kwa wazazi na walezi wote kuwaonya watoto wao au vijana wao kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume cha sheria na maadili ya nchi yetu ambavyo vinaweza lupelekea vurugu na uvunjifu wa amani hasa siku ya Oktoba 29 mwaka huu sambamba na hilo jeshi la polisi halitavumilia wala kukubali vitendo vyovyote kinyume cha sheria siku ya uchaguzi.
Aidha,amesema jeshi hilo linawashikilia watu zaidi ya 17 wakiwemo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kwa makosa ya uchochezi mitandaoni na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Pia amewatahadharisha wanadai kulinda kura kuwa jukumu hilo ni la jeshi la polisi kwa mujibu wa katiba hivyo wananchi wakimaliza kupiga kura waondoke wakaendelee na majukumu yao kama kawaida wataitwa wakati wa kutangaza matokeo .

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako