July 5, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Mbeya yakamata wanachuo wanne kuhamasisha vurugu

Na Mwandishi wetu, TimesmajiraOnline,Mbeya

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wanachuo wanne, wakiwemo viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Elimu ya Juu (CHASO) mkoani humo, kwa tuhuma za kuhamasisha vitendo vya vurugu na uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Julai 5, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amesema watuhumiwa hao walikamatwa Juni 4, 2026, majira ya saa 10:00 jioni katika eneo la Mafiati, Kata ya Iyunga, jijini Mbeya.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kukamilishwa ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Kamanda Kuzaga amewataja waliokamatwa kuwa ni Noah Mwalwange, Mwenyekiti wa CHASO Mkoa; Gwamaka Mboka, Katibu wa CHASO Mkoa; Agustino Wasinyo, Mwenyekiti wa Tawi la CHASO katika Chuo cha CUoM; pamoja na Rojas Mpwani, ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Kamanda Kuzaga amewataka wananchi kuacha kupanga au kushiriki vitendo vya uhalifu, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vinavyohatarisha usalama na amani ya nchi.