December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Paul Nonga afunguka kurudisha pesa za Namungo

Straika mpya wa Gwambina FC Paul Nonga ilimlazimu arudishe nauli kwa mabosi wa Namungo ambao walikuwa wanahitaji saini yake.

Nyota huyo aliyekuwa Lipuli, alikuwa anahitajika kwenda kusaini Namungo kabla ya Gwambina FC kumvutia kasi na kumpa mkataba.
Nonga amesema kuwa awali alikuwa kwenye mazungumzo na Namungo iliyokuwa na nia ya kupata huduma yake, lakini alibadili maamuzi baada ya Gwambina kumfuata rasmi.

“Nilikuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na Namungo ila Gwambina walipoonyesha nia niliwaelewa na nikaenda kusaini, kwa kuwa nilitumiwa nauli na Namungo ilinibidi niwarudishie mkwanja wao,” alisema Nonga