May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Othman akutana na wadau wa maendeleo, CDC na UNAIDS

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Leo Machi 12, 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo kutoka Mfuko wa Rais wa Marekani (PEPFAR); Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Maradhi cha Marekani (CDC); na Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloratibu Masuala ya UKIMWI Duniani (UNAIDS).

Washirika hao wa Maendeleo ambao wamefika kwaajili ya kujitambulisha na kueleza Umuhimu wa Utaratibu wa Mataifa Duniani kote, wa Kuwa na Mipango Endelevu ya Maradhi ya UKIMWI; sambamba na Kutafakari Njia Bora za Kupambana na Kuutokomeza Ugonjwa huo ifikapo 2030 hapa Nchini, wamekutana hapo katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Migombani, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.

Viongozi mbali mbali wameshiriki katika Mkutano huo wakiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Harusi Said Suleiman; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Fedha na Mipango, Dr. Saada Salum Mkuya; Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh; na Mkurugenzi Mtendaji Tume ya UKIMWI Zanzibar, Ahmed Mohamed Khatib.

👆Matukio mbalimbali katika picha