Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online Mbeya
KAMPUNI ya Oryx Gas imesema itaendelea kuiunga mkono Taasisi ya Tulia Trust katika mashindano ya riadha inayoyaratibu kwa kuwa malengo yake yanafanana na ya kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite ameeleza hayo leo Mei 6,2023 baada ya kuwaongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kushiriki mashindano ya riadha yaliyoratibiwa na Taasisi ya tulia Trust na yaliyofanyika jijini Mbeya.
Amesema kuwa Oryx Gas kwa kipindi kirefu imejikita katika huduma za jamii hususani zinazohusu kuisaidia jamii ya Watanzania na zaidi mtoto wa kike kwa kuhakikisha anaondokana na changamoto mbalimbali ,hivyo wameona iko haja kuungana na Tulia Trust katika kumsaidia mtoto wa kike katika afya na elimu ndani ya Mkoa huo.
Akieleza zaidi kuhusu ushiriki wao katika mbizo hizo Araman amefafanua Oryx Gas imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kumuondolea changamoto mwanamke ,hivyo kwenye mashindano ya mbio hizo ni wazi malengo ya taasisi hiyo yanafanana na yao,hivyo wataendelea kuunga mkono.
Amefafanua katika kutekeleza hilo kwa vitendo Kampuni ya Oryx imekuwa na kampeni ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kugawa majiko na mitungi ya gesi kwa wanawake wa mikoa mbalimbali ambapo hadi sasa wamewafikia zaidi ya 5,000, lengo ni kuhakikisha wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa.
“Hivyo tunapoona Taasisi ya Tulia Trust inandaa mbio za kuchangisha fedha kuisaidia jamii ya mtoto wa kike, sisi tunaona ni wajibu wetu kusaidia kwa kufadhili ili mambo yaende kama yalivyopangwa na fedha zinazopatikana zinakwenda kugusa maisha ya wenye uhitaji, tutaendelea kushirikiana na taasisi hii itimize malengo yake,” amesema
More Stories
Maono ya Rais Samia yanavyozidi kuipaisha Tanzania kupitia utalii
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini