November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ORYX, Equity waunga mkono serikali matumizi nishati safi

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam, Timesmajira

BENKI ya Equity na Kampuni ya Gesi ya Oryx zimekubaliana kuiunga mkono Serikali kuhusu matumizi ya nishati safi, ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.-Rais Samia Suluhu Hassan jana Mei 8, 2024 alizindua mkakati wa taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2033.

Akizungumza leo Dar es Salaam katika hafla ya utilianaji saini wa mkataba endelevu, Mkurugenzi wa Equity, Isabela Maganga amesema lengo la makubaliano hayo kwanza kutunza mazingira, kuepuka ukataji miti, lakini kuhakikisha jamii inabadilisha mfumo wa maisha na kuepuka matumizi ya mkaa.

“Tunataka tuhakikishe kwanza tunabadilisha mfumo wa maisha na watu wanaweza kutumia nishati safi, ili kutunza mazingira yetu kuhakikisha kizazi cha sasa na baadaye kinakuwa salama” amesema Isabela.

Isabela amesema katika kuhakikisha gesi inafika maeneo mengi nchini, benki hiyo imekuja na bidhaa ya ‘Distributor Financing’ ambayo inawezesha wakala au msambazaji kupata mkopo kupitia simu ya mkononi.

” bidhaa hiyo imetengenezwa wena kushirikiana na Oryx inawezesha sasa wakala kuongeza mtaji na kununua mzigo mkubwa, uzuri ni kwamba mteja wetu anaipata kwa njia ya kidigitali, haina mlolongo wa kuja benki, baada ya kufanya usajili wa awali anaingia kwenye mfumo wetu malipo kwenye ‘app’ kwa kutumia *150*07#,” amesema Isabela.

Amesema lengo lao ni kuhakikisha wasambazaji wote wanapata bidhaa hiyo kwa urahisi na kuwafikia watumiaji wa mwisho katika maeneo mbalimbali nchini kote.

Aidha, Mkurugenzi wa Orxy, Ashery Mbasha amesema watanataka kuhakikisha gesi inawafikia watu wengi zaidi kwa gharama nafuu, huku wakihakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishafi safi.

Mbasha ametoa wito kwa wasambazaji wengine wa gesi kuhakikisha lengo hilo linatimia ili kuwezesha Watanzania wengi kutumia nishati hiyo.-“Hii bidhaa ina faida nyingi na sisi kama Orxy kwa sababu sisi ndio wasimamizi wakuu wasambazaji wetu tumeona wakitumia sana kwa sababu ya urahisi haikuhitaji kuja benki ukiwa na makaratasi, kupitia tu simu yako unaweza kupata huo mkopo,”amesema Mbasha.

Amesema lengo lao kuhakikisha gesi inawafikia watumiaji wengi kwa bei rafiki, hivyo wataendelea kuhakikisha wanasambaza zaidi na kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.

Mkuu wa Biashara wa Benki ya Equity, Leah Ayubu ametumia nafasi hiyo kutambulisha bidhaa ya Eazzystock Financing ambayo inarahissha upatikana wa bidhaa mbalimbali ikiwemo ya gesi, ambapo amesema mpaka sasa wamefanya biashara na wasambazaji 19.

“Kama wee ni msambazaji tayari unajulikana au ushafanya kwa miezi 12 kwa muda huo Orxy wanakuwa washajua mauzo yako na washakuamini, kupitia hapo Equity tukiona mauzo yako kwa muda huo matokeo mazuri tunaweza kukupa mkopo kulingana na mauzo yako kuanzia Sh milioni 1 mpaka Sh milioni 300.

Kwa upande wa Meneja wa Mauzo wa Benki hiyo, Shaban Fundi Wannmini amesema uwezeshaji wa wasambazaji wakuu unaenda kusaidia upatikanaji wa gesi katika maeneo mbalimbali.

“Kikubwa sio kuwezesha distributor peke yake ni kuwezesha upatikanaji wa gesi nchini katika maeneo mbalimbali nchini,” amesema Fundi.