Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Cristiano Ronaldo ameisababishia hasara ya mabilioni ya dola za Kimarekani kampuni inayotengeneza vinywaji vya Coca Cola baada ya kuondoa chupa za kinywaji hicho mbele yake wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Kitendo hicho kilichosababisha hasara kiliadhiri hisa za kampuni hiyo kushuka kwa kiasi cha dola za Marekani Bilioni 4.
BOFYA CHINI KUTAZAMA VIDEO…
Kwa mujibu wa video iliyowekwa na mtandao wa gazeti la kila siku la Uingereza juzi(16/06/2021), The Guardian na kusambaa katika mitandao mbalimbali haswa ya jamii, ilimuonesha Ronaldo akiondoa chupa mbili za kinywaji cha Coca Cola mbele yake wakati akiwa katika mkutano na waandishi wa habari na kisha kuinua chupa ya maji na kusema kwa Kireno “kunywa maji, Coca Cola…”
Coca Cola ndio mdhamini mkuu wa mashindano ya Euro 2020, ilitoa tamko na kusema kila mtu ana uhuru wa kunywa kinywaji anachotaka, kwa mahitaji yake na mapenzi yake.
More Stories
BAKWATA yawazawadia washindi wakuhifadhi Qur’an
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya