December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ole Sabaya aachiwa huru

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mahakama kuu Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi.

Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.