April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ofisi ya Waziri Mkuu yashiriki wiki ya Utumishi wa Umma

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu waaswa kuendelea kufuata maadili ya utumishi Umma kwa kufanya kazi vizuri na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi, ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Dkt. John Jingu wakati wa semina kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Mjini Dodoma katika Kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma; yenye kauli mbiu “Nafasi ya Mapinduzi ya nne kwa viwanda katika Masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshwaji wakati na baada ya janga la corona.”

“Serikali kupitia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani imeshatimiza wajibu wake kwa kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi; marupupu, vitendea kazi vinapatikana, jukumu letu ni kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia huduma wanayopatiwa na serikali alisema, Dkt Jingu”

Alifafanua vikao hivi ni muhimu vinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kuweza kujua mipaka ya kiutendaji wa kazi iko wapi. Lazima tufanye kazi kama timu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu akizungumza katika semina ya watumishi wa Ofisi hiyo Uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wa idara mbalimbali wakifuatilia semina iliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini Dr. Revocatus Baltazary Ofisi ya Mganga Mkuu Jiji la Dodoma (hayupo pichani) katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Charles na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya wakifutilia kwa umakini semina ya wafanyakazi kwa watumishi wa wizara hiyo iliyofanyika ukumbi wa tume ya Uchaguzi Dodoma