November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NSSF ilivyoshiriki katika maonesho ya wiki ya huduma ya fedha kitaifa jijini Mwanza

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulishiriki katika maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha Kitaifa katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.

NSSF ilitumia maonesho maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, matumizi ya mifumo ya TEHAMA kwa mwanachama na mwajiri ili kumrahisishia huduma bila kulazimika kufika katika ofisi za NSSF, kusikiliza na kutatua kero za wanachama na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo miradi ya nyumba za kisasa, miradi ya uwekezaji ya majengo ya Mzizima Tower na Mwanza pamoja na viwanja.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Utalii Mwanza waliofika katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Festo Fute (wa pili kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Kahensa (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Hifadhi ya Jamii, Omary Mziya (wa kwanza kushoto) na Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Flora Ndutta (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya viongozi hao kutembelea Banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande, (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Flora Ndutta (kulia), kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko katika banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza Flora Ndutta (kushoto), akitoa huduma kwa wananchi waliofika katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza. (wa pili kushoto) ni, Mhasibu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Said Othman Mfuru.
Afisa TEHAMA wa NSSF, Janeth Bwire, akitoa maelezo kwa mwanachama jinsi ya kujihudumia kupitia simu yake kupitia mfumo wa WhatsApp chatbot. Huduma hiyo inapatikana kwa njia ya Whatsapp ambapo mwanachama halazimiki kufika Ofisi katika ofisi za NSSF. Elimu hiyo ya jinsi ya kutumia mifumo inatolewa katika banda la NSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Afisa Matekelezo Mwandamizi, sekta isiyo rasmi Diagi Janguo akimwandikisha Mwanachama mpya wa NSSF alipotembelea banda la NSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Afisa Usalama Mwandamizi wa NSSF,Mfaume Kambangwa akitoa elimu kwa wanachama wa NSSF waliotembelea banda la NSSF namna Mfuko unavyopinga vitendo vya rushwa na kuwa huduma zote zinatolewa bure. Elimu hiyo ya kupinga rushwa katika maeneo ya kazi inatolewa katika Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.