May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Spika Dkt.Tulia awataka UVCCM kubishana kwa hoja ili kuendelea kudumisha amani

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kutumia nafasi zao kubishana kwa hoja na kuendelea kudumisha amani,umoja na mshikamano Hali itakayosaidia kuwalinda Viongozi wa taifa .

Amesema ikiwa vijana hao wataenzi amani na mshikamano itawasaidia kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya na kuwa na Ari ya kufanya kazi kwa bidii .

Dkt.Tulia ameyasema hayo Leo Jijini Dodoma Novemba 26,2022 wakati akifungua mbio za vijana wa UVCCM Katika viwanja vya Jamhuri na kuongeza kuwa ni jukumu la vijana hao kuacha malumbano na kubishana kwa hoja zinazojenga .

Aidha mbio hizo za marathoni kuelekea uchaguzi Mkuu wa UVCCM ngazi ya Taifa unatarajiwa kufanyika Novemba 27,2022 Jijini Dodoma

Spika Tulia amesema,”Hakikisheni Katika chaguzi zenu mnaenzi amani kama  ilivyo itikadi ya Chama chetu,msianzishe vihoja Bali hoja zitakazoeleza maendeleo yanayofanywa na Serikali na si vinginevyo,”amesema

Pamoja na hayo ameeleza kuwa vijana hao Wana jukumu kubwa la kuwalinda viongoi wao kwa hoja zinazoeleweka ikiwa ni pamoja na kuelrkeza mambo mengi yanayofanywa na Serikali.

“Msikae kimya,tangazeni miradi tuliyonayo achañeni kabisa na masuala yanayowapotezea muda ambayo hayajengi,Kuna wakati mnasubiri mtu atoe hoja Ili muanzishe nguvu kuleta  vioja vyenu naomba muache hiyo tabia kwani sio utamaduni wa Chama chetu ,”amesema

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana wa hamasa wa Chama hicho Kwa juhudi zao Katika kuamsha Ari kwenye matukio ya Viongozi wakuu na kueleza kuwa huo ndio Uzalendo unaotakiwa Kwa Kila kijana.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM )Kenani Kihongosi amemshukuru spika Tulia Kwa kukubali kuungana nao katika mbio hizo zilizoambatana na matembezi ya amani.