January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yatoa mil.26 kuinua sekta ya elimu,afya Tabora

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Sikonge

BENKI a NMB imetoa zaidi ya shilingi milioni sh.26.2 kusaidia sekta ya elimu na afya wilaya za Tabora na Sikonge .

Benki hiyo imetoa msaada wa madawati 100 na viti vyake yenye thamani ya shilingi milioni 10,katika shule za Sekondari za Ipuli na Intonjanda ambapo kila shule imepata madawati 50.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge John Pallangyo(Wakwanza Toka Kushoto), akipokea Vifaa vya Afya, Mashuka na Vitanda kutoka kwa Sospeter Magese Meneja wa Nmb kanda ya magharibi. Benki ya NMB wiki imekabidhi vifaa vyenye thamani ya milioni 26 wilaya ya sikonge na Tabora ikiwa utekelezaji wa mpango wa uwajibikaji kwa jamiii.

Katika Wilaya ya Sikonge,NMB imetoa madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milioni 4.2 katika shule ya msingi Mbirani na madawati na viti 50 katika shule ya Sekondari Kiwele yenye thamani ya shilingi mil.4.7 pamoja na Vvfaa mbalimbali kama vitanda,magodoro an mashuka katika hospitali ya Wilaya ya Sikonge vyenye thamani ya shilingi milioni 7.3.

Meneja wa NMB Kanda ya magharibi,Sospeter Magese,Akizungumzia msaada huo,amesema NMB imetoa msaada huo kwa vile inathamini elimu na Afya kwani Taifa lisiloweka jitihada katika sekta hizo haliwezi kupata maendeleo.

“Tutaendelea kusaidia kutoa misaada katika sekta za elimu na Afya ikiwa tunaendeleza utaratibu wa kurudisha sehemu ya tunachopata kwa jamii” amesema.

Magese ameeleza kuwa watasaidia pia kuezeka maboma ya shule kama wataombwa kusaidia pale ambapo halmashauri zimeshindwa kumalizia maboma ya shule.

Akipokea msaada wa madawati 100 kwa shule za Sekondari za Ipuli na Intonjanda,mkuu wa Wilaya ya Tabora,Dkt. Yahaya Nawanda,ameshukuru NMB kwa msaada huo,amesema utasaidia wanafunzi kuandika vizuri na kufanya vizuri kwenye masomo Yao.

Amewataka wanafunzi hao,kuongeza bidii katika masomo Yao na kudhihirisha thamani ya msaada waliopewa na benki hiyo.

Pia ametoa wito kwa wazazi,watumishi wa Serikali na wanafunzi,kuitumia benki ya NMB kwa vile mbali ya kusaidia jamii pia inatoa bima mbalimbali zenye manufaa kwa wananchi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Sikonge,John Pallangyo,mbali ya kuishukuru NMB kwa msaada wa madawati 100 kwa shule za Kiwele na Mbirani pamoja na Vifaa hospitali ya Wilaya,Alisema hawatabweteka Bali kuongeza jitihada zaidi ili kutatua changamoto za miundombinu ya shule kwenye wilaya hiyo.

Pia amesema watatoa vibali kwa watu kuvuna miti kwa ajili ya kutengeneza madawati kwa vile ni aibu kuwa na misitu mingi wakati Wana upungufu wa madawati.

Kutoka Kushoto ni Wanafunzi 2 Shule ya Mbilani Sikonge, anaefuata Mkuu wa Wilaya ya Sikonge John Pallangyo (Mwenye barakoa), Meneja wa Nmb kanda ya magharibi Sospeter Magese  (Mwenye Suti ya Bluu Katikati na Barakoa) anaefuata ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Rashidi Magope na wa Mwisho ni Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Sikonge Tito Luchagula.


Kwa Upande wao Wakuu wa Shule za Ipuli Sekondari Wilaya ya Tabora Faines Msigara na Ally Baruani Mkuu wa Shule ya Msingi Mbilani Walaya ya Sikonge, Wameishukuru Benki ya NMB kwa Msaada huo wa Madawati Kuwa Utasaidia Wanafunzi Kusoma kwa nafasi Kutokana na Upungufu wa Madawati Uliokuwepo.

Benki ya NMB imekuwa ikitoa misaada ya elimu na Afya kwa shule na vituo vya kutolea huduma ambapo katika Kanda ya magharibi Kuna mi koa ya Simiyu,Shinyanga,Kigoma na Tabora