January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yatoa elimu ya huduma zao kwa wananchi Wiki ya Huduma ya Kifedha jijini Mwanza

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Bi. Vicky Bishubo (kushoto), alipotembelea banda lao na kumuelezwa kuhusu jitihada zao walizofanya kutoa Hati Fungani ya ‘Jasiri Bond’ ambapo jumla ya Sh. bilioni 74.3 zilipatana kwa ajili ya kuwawezesha akina mama wanaofanya shughuli za kiuchumi kwenye sekta ndogo na za kati hapa chini.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Ndg. Lawrence Mafuru (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo katika viwanja vya Rock City jijini Mwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo, katika viwanja vya Rock City jijini Mwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) Tuse Joune (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa NMB, Vicky Bishubo jijini Mwanza wakati wa maonesho ya wiki ya Huduma za Fedha kitaifa.