Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi -Zanzibar imeipongeza Benki ya NMB kwa kuleta masuluhisho maalum yalio rafiki kwaajili ya wakandarasi huku akiamini ndio njia rahisi ya kusaidia kuwakuza wakandarasi wazawa kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed alipokuwa anazindua rasmi warsha ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi wa Zanzibar ikiwa na lengo la kuwatambulishia suluhisho mpya kwaajili ya wakandarasi na kuwasihi wachangamkie fursa hizo.
Mbali na hilo, Waziri huyo aliwasihi pia wakandarasi kutumia fedha za mikopo wanaopata kutoka kwa mabenki kwaajili ya kazi waliokopea na sio kwa shuguli zingine kwa inaweza wapa ugumu katika kurejesha mkopo huo.
Akizungumza katika warsha hiyo, mwakilishi wa Benki ya NMB ambae ni Mkuu wa Idara ya Miamala wa Benki hiyo, Bi. Linda Teggisa alisema kuwa Benki ya NMB imesimama katika nafasi ya kuendelea kuongeza fursa ya upatikanaji wa huduma za kifedha ili kuendelea kuwawezesha wakandarasi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za dhamana za zabuni kwaajili ya miradi au manunuzi (unsecured bid bond) pamoja na dhamana za utekelezaji (performance guarantee) au dhamana za malipo ya awali (advance payment guarantee), zote ambazo hazihitaji dhamana.
Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkuu wa wilaya ya Mjini, Mhe. Komred Rashid Simai Msaraka alisema kuwa sekta ya ujenzi imekuwa ni sekta ya muhimu sana kwa Zanzibar kwa sasa kwani ni miongoni mwa Sekta ambazo zinaongeza ajira zilizo na zisizo rasmi kwa wananchi wa Zanzibar na kupongeza taasisi za fedha kuamua kuongeza nguvu kwa sekta hii sio tu kuwanyayua wakandarasi lakini linaenda kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa Zanzibar.Â
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano