November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Njombe TC waeleza fursa za kilimo na ufugaji

Na Yusuph Mussa, TimesMajira Online, Mbeya

HALMASHAURI ya Mji Njombe (Njombe TC) katika Mkoa wa Njombe, imetangaza fursa za kilimo na ufugaji zilizopo kwenye halmashauri hiyo, ambapo ina eneo la hekta 321,200, huku linalofaa kwa kilimo ni hekta 192,700, na linalolimwa kwa sasa ni hekta 32.7 bila kuingiza kilimo cha miti na mazao ya misitu.

Hayo yalisemwa Agosti 8, 2022 na Ofisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Henry Kideula kwenye Banda la Maonesho ya Nane Nane lililopo mjini Mbeya, na kuongeza kuwa, takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa ukubwa eneo la uzalishaji chakula, mahindi ni hekta 26,700, ngano hekta 1,982 na ulezi hekta192.5.

Maharage hekta 2,596, njegere hekta 1,561, viazi mviringo hekta 22,660, na viazi vitamu hekta 1,097, na jumla kuu hekta 56,787.5. Na halmashauri hiyo, ina mazao ya chakula ambayo ni mahindi, ngano, ulezi, maharage, njegere, viazi mviringo na viazi vitamu, huku mazao ya biashara yakiwa ni parachichi, chai na matofaa (apple).

Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2022 ni mahindi tani 109,404.13, ulezi tani 555.35, ngano tani 7.776.60, viazi vitamu tani 5,430.15, viazi mviringo tani 396,602. 50, maharage tani 7,277.20 na njegere tani 4,413.70, na jumla ni tani 526,459.63.

“Eneo la uzalishaji wa mazao ya biashara mwaka 2022, parachichi ni hekta 1,764, chai hekta 4,200 na matofaa (apple) hekta 169.4. Na uzalishaji mazao ya biashara ni parachichi tani 2,200, chai tani 5,040 na matofaa (apple) tani 89.73” alisema Kideula kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick.

Naye Ofisa Mifugo wa Halmashauri hiyo Thadei Luoga alisema eneo linalofaa kwa malisho ni hekta 48,802, ambapo hekta 36,601.50 zinatumika kwa malisho wa ng’ombe wa asili na hekta 190 ni malisho wa ng’ombe wa kupandwa.

Wakati idadi ya mifugo kwenye halmashauri hiyo, ng’ombe wa asili ni 18,387, ng’ombe wa maziwa 3,163, mbuzi 13,142, mbuzi wa maziwa 16, kondoo 3,959, nguruwe 19,713, mbwa 5,225, punda 2,934, paka 7,110, simbilisi 29,205, sungura 8,625, kuku wa asili 51,889, kuku wa kisasa 272,419, bata mzinga 215, kwale 23, njiwa 679 na farasi saba.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe Kuruthum Sadick (kulia) akipata maelezo ya ufugaji bora wa kuku kwenye Banda la Halmashauri ya Mji Njombe katika Maonesho Nane Nane mkoani Mbeya. (Picha na Yusuph Mussa).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe Kuruthum Sadick (kulia) akipata maelezo ya ufugaji bora wa samaki kwenye Banda la Halmashauri ya Mji Njombe katika Maonesho Nane Nane mkoani Mbeya. (Picha na Yusuph Mussa).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe (TD) Kuruthum Sadick (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe (DED) Sharifa Nabalang’anya (kushoto) na Ofisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga (kulia), wakibadilisha mawazo mara baada ya kukagua Banda la Halmashauri ya Mji Njombe katika Maonesho Nane Nane mkoani Mbeya. (Picha na Yusuph Mussa).
Ofisa Kilimo Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe Henry Kideula (kulia) akionesha mahindi yaliyopandwa kwenye banda la Maonesho ya Nane Nane la halmashauri hiyo mkoani Mbeya. Kushoto ni Mratibu wa Nane Nane upande wa kilimo wa halmashauri hiyo Filingson Kajun. (Picha na Yusuph Mussa).