December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nike wavunja Mkataba na Kobe Bryant

LOS ANGELES, Marekani

KAMPUNI ya Nike umevunja Mkataba na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu katika timu ya Los Angeles Lakers Kobe Bryant, huku kampuni hiyo ikikataa kuongeza tena.

Kwa mujibu wa USA TODAY Kampuni hiyo imethibitisha kuwa, Mkataba na mchezaji huyo wa zamani uliisha licha ya kuwa na mahusiano mazuri kipindi alipokuwa akiichezea Lakers.

“Kobe Bryant alikuwa sehemu muhimu ya uhusiano wa kina wa Nike kwa watumiaji. Alitusukuma na kufanya kila mtu aliye karibu naye kuwa bora. Ijapokuwa uhusiano wetu wa kimkataba umeisha, yeye bado ni mtu wa kupendwa sana wa familia ya Nike,” imesema taarifa kutoka Nike.

Haijafahamika mara moja ni sababu gani zilizochangia uhusiano uliofutwa. Bryant, ambaye alisaini na Nike mnamo 2003 baada ya kuwa mteja wa adidas, alihusika sana na maono na muundo wa viatu vyake.

Tangu alipofariki Januari 26, 2020, mjane wa Bryant, Vanessa, amesimamia mambo yake kadhaa ya kibiashara. Vanessa amehusika na “Granity,” kampuni ya kusimulia hadithi ambayo Bryant alianzisha.