May 11, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NEW YORK, NEW YORK - FEBRUARY 05: Kevin Durant #7 of the Brooklyn Nets reacts after he is called for a foul in the second half against the Toronto Raptors at Barclays Center on February 05, 2021 in New York City. After a coach's challenge the call was overturned and Durant was not charged with a foul. Durant left the court after contact tracing determined he had contact with someone who tested positive for Covid-19. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and or using this photograph, User is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. (Photo by Elsa/Getty Images)

Brooklyn Nets yapata pigo kwa Durant

MIAMI, Florida

TIMU ya Kikapu ya Brooklyn Nets imepata pigo, baada ya Nyota wake Kevin Durant kupata jeraha kwenye paja lake la kushoto, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani NBA, uliofanyika mwishoni mwa wiki dhidi ya Miami Heat.

Katika mchezo huo ambao Miami iliibuka na ushindi wa vikapu 109-107, Durant alitoka nje dakika 7:57 katika robo ya ufunguzi huku akifunga alama nane za kwanza za mchezo kabla ya kutoka, na baadaye timu hiyo ilitangaza mchezaji huyo hawezi kurejea dimbani.

Akizungumzia hilo kocha wa Nets Teve Nash amesema, Durant amepatwa na jeraha la paja lakini hatufahamu ameumia kwa kiasi gani ila tutafahamu atakapofanyiwa vipimo.

Durant, mwenye umri wa miaka 32 raia wa Marekani, amekosa michezo 33 msimu huu, na 24 kati ya hiyo inahusiana na jeraha la mguu wa kushoto. Alikosa mingine kutokana na kukaa katantini kwa sababu ya kukutwa virusi vya corona.

Mbali na mchezaji huyo, Nets walicheza bila ya nyota wake James Harden kutokana na kusumbuliwa na misuli pamoja na Jimmy Butler akisumbuliwa na mguu.