Na Joyce Kasiki, Dodoma
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imepata mtambo mpya wenye uwezo wa kuzalisha vitambulisho 9,000 kwa saa .
Mtambo huo umenunuliwa ili kumaliza kero ya upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa ambavyo havipatikani na badala yake watu wamekuwa wakipatiwa namba za nida tu baada ya kujisajili na kutambuliwa.
Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini hapa, waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene alisema, kiasi hicho cha fedha kimetolewa na Rais John Magufuli ili mamlaka hiyo izalishe vitambulisho hivyo kulingana na mahitaji.Alisema, Serikali iliweka matarajio ya kuwatambua na kuwasajili wananchi milioni 27.7 anbapo hadi kufikia Machi 2020 wananchi milioni 21.8 walikuwa wamesajiliwa .
Alisema hadi kufikia machi 27 mwaka huu jumla ya namba za kipekee za utambulisho wa Taifa milioni 17.8 zilikuwa zimezalishwa lakini waliopata vitambulisho halisi ni wananchi milioni 6 tu.
“Nikiri kwamba hapo kuna uzembe ulijitokeza kwa watumishi ambapo walishindwa kutumia mashine kwa uangalifu,walizitumia bila kuzifanyia ‘service’ na matokeo mtambo ulishindwa kuzalisha kwa kasi iliyokusudiwa.”alisema Simbachawene.
Hata hivyo alisema,mtambo huo mpya utaiwezesha mamlaka hiyo kuzalisha vitambuylisho hivyo kwa kasi ambapo ndani ya kipindi cha miaka miwili wananchi wote watakuwa wameshasajiliwa.
Alisema mtambo huo mpya utafungwa msihoni mwa mwezi April mwaka huu na vitambulisho vitaanza kuzalishwa kwa kasi.
“Mtambo huu utaanza kufanya kazi pamoja na ule wa zamani ,kwa hiyo hapa najua kasi itakuwa kubwa kwani vitambulisho vitazalishwa kwa wingi zaidi “alisisitiza
Waziri Simbachawene alitumia fursa hiyo kuwaomba radhi wananchi kutokana na changamoto walizozipata katika zoezi hilo ikiwemo kutolewa lugha chafu na watumishi wa Nida waliopo wilayani wakitekeleza zoezi hilo.
Alisema,katika baadhi ya wilaya wananchi hawajahudumiwa vizuri na watumishi wa Nida huku akiwataka watumishi hao hususan waliopo mipakani ,kufanya kazi zao kwa kushirikisha uongozi wa Serikali za mitaa.
“Kuna baadhi ya watumishi walitoa luigha mbaya kwa wananchi kwa kuwamaambia wao siyo raia,sasa hii siyo lugha nzuri,na wao hawawezi kufanya kazi hiyo pekee bila kushirikisha uongozi wa Serikali za mitaa ambao wao ndio wanawafahamu wananchi kwani wanaishi nao na hivyo wanajua nani raia na nani siyo raia.”alisema
Amewataka Wakuu wa Mikoa ,wakuu wa wilaya na Makatibu Tawala kuhakikisha wanawasimamia watumishi wa Nida pindi wanapofanya kazi ili wasiojione kama wao wanaweza kufanya na kuwajibu wananchi vyovyote wanavyotaka wao.
“Hawa viongozi wote ni mamlaka zinazotambulika hivyo wanao wajibu wa kuhakikisha wanawasimamia watumishi wa Nida ili wasiweze kuwajibu wananchi vile wanavyotaka wao na kujifanya muingu watu.”alisisitiza Lengo la Serikali lilikuwa ni kuwafikia wananchi wote kwa kuwasajili , kuwatambua na kuwapa kadi halisi mwaka 2020.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao