May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NHC yatoa msaada kwa wenye uhitaji

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

TAASISI ya haki sawa kwa watu wenye ulemavu ya ‘Equal Rights for People with Diabilities’ imelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) kwa msaada wa fimbo kwa watu wenye ulemavu wa macho, vifaa saidizi kwaajili ya viwiko, mafuta ya kukinga ngozi dhidi ya miale mikali ya jua na vifaa saidizi kwaajili ya mwendo.

Akizungumzia Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Said Mrisho Halilli, muda mchache baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo na timu kutoka NHC, makao makuu ya Chama hicho Mtaa wa Kanuni, Mabibo, Dar Es Salaam.

“Mungu, awabariki sana NHC, hii siyo mara kwanza kufanya hivi, mmekuwa Kimbilio letu na huwa hamtuachi, mmekuja wakati muafaka sana ikizingatiwa kuwa hiki ni kipindi cha mvua ambacho kina changamoto sana hususani kwenye suala la mwendo Kwa watu wenye ulemavu, alisema Makamu Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Equal Rights for People with Diabilities.

Katika hatua nyingine, Taasisi hiyo imetoa wito kwa Mashirika ya Umma kama NHC na ya Sekta binafsi, kuiga mfano wa NHC kwa kutoa msaada huo bila kusubiri msimu wa sikukuu ama maadhimisho husika, kwakuwa mahitaji yao ni ya wakati wote.

Kwa upande wa NHC, Yahya Charahani, ambaye ni Afisa Uhusiano Mkuu kutoka kitengo cha Uhusiano na Habari, cha Shirika hilo, akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, amesema, ni utaratibu wa NHC, wa kurejesha kidogo inachopata kwa jamii lakini kubwa ni utekelezaji wa kisheria wa suala hili kwa lugha ya kimombo Corporate Social Responsibility ( CSR).