Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) katika kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi limetoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya milioni 5 kwa hospitali ya rufaa ya mnazi moja Zanzibar.
Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa ni pamoja na floor meter, patients stand monitor, patients monitor, pulse oximeter, breathing system za anesthetic machine, patients screen ikiwa ni sehemu ya kurudisha huduma kwa Jamii.
Ameyasema hayo Leo oktoba 13, 2023 Zanzibar, Afisa Habari na Uhusiano – NHC, Domina Rwemanyila wakati akikabidhi vifaa tiba kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa mnazi mmoja Zanzibar Abdallah Haji.
Rwemanyila Amesema kuwa msaada huo wa vifaa tiba kwa hospitali ya mnazi moja Zanzibar ni muendelezo wa shughuli zinazofanywa na shirika la nyumba la Taifa – NHC katika kuendelea kutoa huduma kwa Jamii.
Aidha, ameongeza kuwa msaada huo utaendelea kuongeza kushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na shirika la nyumba la Taifa ikiwa ni pamoja na kuunga mkono Juhudi ya SMZ inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa mnazi mmoja Zanzibar Bw. Abdallah Haji amesema kuwa wamefarijika sana kuona wenzetu wa shirika la nyumba la Taifa wameguswa na kuona ipo haja kwa njia Moja au nyingine katika kushiriki kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar.
“Jambo hili ni muendelezo wa wadau mbalimbali kwa nafasi zao huwa wanauliza mahitaji katika hospitali ya rufaa mnazi moja Zanzibar kwa lengo la kutoa misaada au kuchangia ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia jamii kupata huduma ya Afya”. Amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa mnazi mmoja Zanzibar Bw Abdallah Haji
Hivyo, tunapokea misaada tofauti ikiwemo dawa, vifaa tiba na wakati Mwingine tunawapatia wagonjwa mbalimbali vyakula, maji pempas kwa watoto na vinginevyo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi