December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NHC kushiriki kuboresha miundombinu ya michezo nchini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu amekutana na na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah ambapo wamejadiliana namna kuendeleza ushirikiano baina ya pande mbili ili kuendeleza miundombinu ya michezo nchini.

Kikao hicho kimefanyika Juni 07, 2023 katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatekeleza miradi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo jengo la ofisi za Wizara linalojengwa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma pamoja na eneo la changamani la michezo Kawe jijini Dar es Salaam.