
Na Israel Mwaisaka, Rukwa.
MAMIA ya wananchi wa Mkoa wa Rukwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha kubwa la Rukwa Ngoma Festival lililofanyika na kutikisa mjini Sumbawanga, ambapo wananchi walipata burudani mchanganyiko wa ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya.
Tamasha hilo lilitumika pia kuanikwa kwa fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazotokana na ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 2026 mkoani hapa.
Akimzungumza katika tamasha hilo, Katibu wa kamati ya hamasa Mkoa wa Rukwa, Khadija Dalasia, aliwahimiza wananchi kujiandaa mapema kunufaika na ujio wa Mwenge wa Uhuru, akibainisha kuwa utavutia wageni wengi na kuchochea mzunguko wa biashara.
Alisema sekta za biashara, usafirishaji na malazi ndizo zitakazonufaika zaidi, hivyo wananchi wanapaswa kutumia ipasavyo fursa hiyo kuongeza kipato chao.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo waliipongeza kamati ya maandalizi, wakieleza kuwa matukio kama hayo yanasaidia kuchochea uchumi na kuamsha sekta ya biashara mkoani Rukwa.

More Stories
JNHPP: Ndoto ya Nyerere yatimia,Rais Samia apongezwa
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino
InnoIP Tanzania yazinduliwa kuimarisha ulinzi wa ubunifu