January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NEMC yampongeza RC Makalla kwa maboresho coco beach

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC limempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla kwa ubunifu wa kuboresha mazingira kwenye ufukwe wa Coco Jambo lililofanya ufukwe huo kwa Sasa kuwa na mandhari nzuri ya kuvutia.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Samuel Gwamaka amesema awali ufukwe huo ulikuwa na mwonekano usioridhisha Kutokana na Vibanda vilivyokuwepo kuwa na taswira mbaya ya matambara na magunia lakini Sasa mandhari imekuwa ya kuvutia baada ya Ujenzi wa Vibanda vya kisasa.

Kutokana na hilo Dkt. Gwamaka amesema Baraza hilo limetenga kiasi Cha Fedha kwaajili ya Ujenzi wa kuta ili kuzuia maji kuendana na Hali ya usalama wa kimazingira.

Aidha Dkt. Gwamaka amesema Baraza limeridhishwa na Hali ya Ujenzi wa Vibanda visivyo vya kudumu na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katika kila maboresho yatakayohitajika.