May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBAA yaendelea kushirikiana na serikali, wadau katika fani ya Uhasibu

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

BODI ya wahasibu Tanzania NBAA imesema kuwa itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wa nje na ndani kuhakikisha Tanzania inakuwa na maendeleo katika fani ya uhasibu, fedha na huduma nyinginezo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya NBAA katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno amesema NBAA imeweza kuishauri Serikali katika masuala ya kodi haswa kwenye maboresho na kuongeza wigo wa kodi na kupunguza ambazo zinaharibu jamii .

Ameeleza kuwa NBAA imeweza kukagua makampuni 402 ya ukaguzi na kampuni za simu 102 na kubainisha kuwa idadi ya Wanafunzi imeendelea kuongezeka ambapo kwa sasa kuna wanafunzi takribani 7000.

Amesema shughuli zote za NBAA zinafanyika kwa mfumo wa tehama isipokua shughuli moja ya usimamamizi wa mitihani kutokana na changamoto ya utamaduni wa Tanzania huku akibainisha kuwa changamoto hiyo inafanyiwa kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Miaka 50 NBAA CPA Dr. Neema Kiure amesema kuwa tokea NBAA imeanza mpaka mwaka huu 2022 wameidhinisha wahasibu 12.000 kati ya hao asilimia 70 ni wanaume na wahasibu 30 ni wanawake, hivyo NBA imekuwa ikitoa kozi mbalimbali kwa wahasibu na kushauri serikali mambo mbalimbali katika uhasibu.

“Katika kuanzishwa kwake mwaka 1972 NBAA imekuwa na viongozi mballimbali na leo tunajivunia, viongozi ambao wameufanya uhasibu Tanzania ufike hapa tulipo” Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Miaka 50 NBAA CPA Dr. Neema Kiure