November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nauli za vivuko zilizopitwa na wakati vyaipa changamoto TEMESA

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

WAKALA wa Ufundi na Umeme (TEMESA)umesema unakabiliwa na Changamoto kubwa kwa sasa ya nauli za vivuko zilizopitwa na wakati, zisizoendana na bei ya soko wala Gharama halisi za uendeshaji wa vivuko pamoja na ulipaji usioridhisha wa wateja wanaohudumiwa na Wakala hasa katika matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo.

Hayo yamesemwa jijini leo,Februari 10 ,2023 na Mtendaji Mkuu wa Wakala huo,Lazaro Kilahala wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli na utekelezaji wa bajeti ya wakala kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Kilahala amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 Wakala ulijipangia kuzalisha jumla ya Shilingi 90,435,876,240 kama mapato ghafi kupitia shughuli zake za Matengenezo na Ufundi, Usimamizi wa Vivuko, Ukodishaji wa Mitambo na Huduma za Ushauri.

 “Utendaji wa Wakala katika mwaka wa fedha 2022/23: Hadi kufikia Disemba 31, 2022 Wakala ulifanikiwa kuzalisha mapato ghafi ya jumla ya Shilingi Bilioni 31.53 sawa na asilimia 35 huku  lengo la mwaka likiwa  kuzalisha Shilingi Bilioni 90.43,”amesema.

Kilahala amesema Utendaji wa Wakala huo uliathiriwa na uchakavu wa vivuko pamoja na mabadiliko ya kiutendaji yaliyotekelezwa na Wakala katika nusu ya kwanza ya mwaka.

Aidha amesema utendaji unatarajiwa kuimarika kadiri mabadiliko yanavyozoeleka na ukarabati wa vivuko unavyokamilika.

Pamoja na hayo Kilahala ametajakazi Kazi zinazoendelea kutekelezwa na Wakala katika mwaka wa fedha 2022/23 kuwa Kusimamia uendeshaji na matengenezo ya vivuko,matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo ya Serikali kupitia mtandao wa Karakana 27 kote nchini, Tanzania Bara.

Nyingine ni usimikaji wa mifumo ya umeme na elektroniki katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa SimiyuUsimikaji wa mifumo ya Umeme na elektroniki katika Jengo la Mama na Mtoto, Hospitali ya Mawenzi Kilimanjaro.

“Usimikaji wa mifumo ya Umeme na elektroniki katika majengo ya Ofisi za Halmashauri ya Miji ya Kahama na Bariadi,usimikaji wa mifumo ya umeme na elektroniki katika kiwanda kipya cha Bohari ya Madawa (MSD) kilichopo Idofi Makambako NjombeUsimikaji wa mifumo ya umeme na elektroniki katika majengo ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora yaliyopo Mji wa Serikali (Magufuli City) Mtumba mjini Dodoma.