May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenza wa Makumu wa Rais Marekani atembelea kituo cha JK Park, Dar

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

Mwenza wa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamalla Haris. Douglas Emhoff leo ametembelea Kituo Cha kukuza Vipaji vya Michezo Jakaya Kikwete Youth Park, kilichopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki pamoja na Mwenza wa Makamu wa Rais wa Marekani Emhoff.

Hata hivyo, Emhoff amepata fursa ya kufanya ziara fupi kuona jinsi kituo hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuzungumza na vijana wanaofundishwa mpira wa Miguu na Kikapu katika Kituo hicho.

Mara baada ya kufanya ziara hiyo, Emhoff amewasihi vijana hao wajifunze kwa hari na Bidii ili waje kuwa nyota wazuri na wakubwa Duniani.

Kwa upande wake, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru Mwenza huyo kwa ziara yake katika Kituo hicho.

Balozi Dkt. Chana amesema, miongoni mwa vituo vinavyolea vipaji ambavyo vinatarajiwa kuisaidia nchi katika Sekta ya michezo.

amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua milango kwa wadau ndani na nje ya nchi kuona fursa zilizopo nchini katika Sekta za Michezo, Utamaduni na Sanaa na kuzitumia katika kuleta maendeleo kwa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango kwa wadau wa nje na ndani katika sekta za michezo, Utamaduni na Sanaa,” amesema Dkt. Pindi Chana.