May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba aipongeza Wilaya ya Ubungo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba ameipongeza Wilaya ya Ubungo kwakuweza kukidhi vigezo katika mradi wa Shule za Sekondari zilizojengwa kwa kutumia pesa za Uviko 19 katika maeneo mengi nchini Tanzania.

Kate ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa umoja wa Vijana (UVCCM) Kata ya Mabibo ambapo amesema hatua hiyo imekuja kutokana na Umoja na mshikamano baina ya viongozi na wakandarasi waliokabidhiwa kazi hiyo.

“Mmefanya kazi kubwa sana nawapongeza naomba muendelee hivi katika mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ubungo mmekua vinara mmekidhi vigezo vyote vilivyokua vikitakiwa katika mradi huu”amesema Kate.

Akijibu suala la ukosefu wa ajira kwa vijana katika Kata hiyo, amewahidi kuwaunga mkono katika kuhakikisha vijana wanaweza kujiajiri wenyewe kwa kubuni mradi wa maendeleo utakaoweza kuwapatia tija na kipato.

“Katika kila Halmashauri kuna pesa zinazoletwa asilimia 10 kwa ajili ya vijana, akina mama na walemavu, kuna sehemu niliona mradi vijana wameanzisha nataka niwachukue vijana hapa niwapeleke muende mukajifunze kama mutaupenda muufanye katika kiwango kizuri zaidi kupitia pesa hizi za Halmashauri”amesema Kate.

Aliwataka vijana hao kutotumika kisiasa na badala yake wachague viongozi ambao ni sahihi na wanauwezo wa kuongoza ili waweze , kuwavusha sehemu moja kwenda nyengine kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.

Naye Diwani wa Kata ya Mabibo Joseph Thomas
amesema kata hiyo imepokea fedha za UVIKO 19 millioni 160 kutoka Serikali kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 8, ambapo madarasa hayo yamejengwa kwa vigezo vilivyokua vinahitajika.

Amesema kuwa, kata ya Mabibo ni moja ya kata 14 zilizoko katika Manispaa ya Ubungo na kueleza kuwa fedha hizo walizopata zimekuja kwa maelekezo ya kutumika kwa wakati.

“Awali darasa moja lilikuwa likibeba wanafunzi 100 hivyo baada ya Ujenzi wa Madarasa hayo kukamilika itasaidia kupunguza msongomano wa wanafunzi”amesema

Kwa upande wake Katibu UVCCM Kata ya Mabibo Raufu Mkonga amesema kuwa, lengo la UVCCM ni kuhakikisha wanaongeza jeshi kubwa la wanachama katika mapambano ya kuilinda na kuitekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo.

Aidha, amesema wanatamani wawe na mradi wa kwao ambao itawezesha kuwasaidia kujiajiri na kupata kipato,kwani suala la ajira imekua changamoto kubwa sana hususani kwa vijana.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam akiwa pamoja na watendaji wa kata ya mabibo wakati wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM)
This image has an empty alt attribute; its file name is WhatsApp-Image-2021-12-31-at-4.59.40-PM-1024x496.jpeg
Diwani wa Kata ya Mabibo Joseph Thomas miongoni mwa Watendaji walioudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM)
Vijana wa UVCCM Kata ya Mabibo wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM)